Wabunge watatu waliokuwa wametembelea watu waoaishi ndani ya msihtu wa Mau wametiwa mbaroni.

Watatu hao akiwemo Johanna Ng’eno wa Emurua Dikir walikamatwa na maafisa wa polisi wanaoshika doria katika msitu huo. Polisi wameweka vizuizi katika barabara zote zinazoelekea katika eneo ambalo serikali imetangaza kuhamisha watu.

Wabunge hao walikuwa wamepenya mtengo wa polisi kwa kutumia pikipiki.

Serikali ilitangaza kufurusha watu wanaoishi katika msitu wa Mau kwa lengo la kuutunza msitu huo. Hatua hii hata hivyo imepingwa vikali na baadhi ya viongozi wa bonde la ufa wakiongozwa na kiongozi wa waliowengi katika seneti Kipchumba Murkomen.

View Comments