- images
- lon_5

Gavana wa kaunti ya Pokot Magharibi Governor John Lonyangapuo amezima stima za uhasama na hasimu wake wa kisiasa Dennis Ruto Kapchok almaarufu kama Mulmwas. Mapema mwakani kipande kifupi cha video kilitamba katika mitandao ya kijamii kikionyesha Gavana huyu akikerwa zaidi na Dennis.

Soma hadithi hii:

"Kijana fupi huwezi jua tumbo iko wapi mgongo ni wapi" ni sauti iliyosikika katika video hiyo. Dennis sasa anasema kuwa yuko tayari kufanya kazi na gavana Lonyangapuo baada ya babake William Lopetakou ,ndugu na marafiki kumshawishi aache siasa za kumpinga.

Mbunge wa Cheliba Peter Nang'ole, mteuliwa wa kuwakilisha wodi na shangazi wake Josephine Cheprum na binamu wake Zacharia Loripo walisaidia pakubwa katika mchakato wa upatanisho.

Soma hadithi hii:

Kapchok sasa anahoji kuwa gavana na serikali ya kaunti wametimiza matakwa aliyokuwa akiyapigania yawepo.

Aisha Dennis alipuuzilia mbali taarifa kuwa amepewa hongo kuacha upinzani na kuunga mkono serikali ya Lonyangapuo

View Comments