maxresdefault__1567664088_50728

Wazo na uamuzi wa chama tawala cha Jubilee kumteua mwanasoka McDonald Mariga kugombea kiti cha ubunge Kibra umejawa na songombingo tele huku wengi katika chama hiki wakihoji uteuzi huu ulikiuka demokrasia. Uamuzi huu sasa unatokota ndani ya chama hiki na huenda ukasababisha utengano.

Soma hadithi nyingine:

Cherangany MP Joshua Kutuny amekuwa wa kwanza kutangaza na kusema kuwa njia iliyotumika kwa kweli inahujumu demokrasia. Kulingana na mbunge huyu, wagombeaji wote 16 walipaswa kufanyiwa mchujo wa kina kabla chama kimtangaze nguli huyu wa soka.

Soma hadithi nyingine:

 Wabunge Moses Kuria (Gatundu South),Maina Kamanda na Joshua Kutuny wametia shaka mchakato mzima wa kumchagua Mariga huku wawili wakitishia kumuunga mkono mgombeaji wa ODM.

Katika chapisho rasmi mtandao wa Facebook, Kuria alisema atamuunga mkono Musungu kwa sababu yeye ni mzaliwa wa Kibra huku akimfananisha na aliyekuwa mbunge wa eneo hilo marehemu Ken Okoth. Alisema kwamba kiongozi aliyezaliwa Kibra anafahamu shida na changamoto za wakaazi wa eneo hilo na ana nafasi nzuri kuboresha maisha ya watu wa eneo hilo.

Soma hadithi nyingine:

“Rafiki yangu Ken Okoth alizaliwa Kibra na alikuwa amejitolea sana kuimarisha maisha ya watu wa Kibra. Mtu ambaye nitapigia debe kuendeleza mipango ya Okoth ni mzaliwa mwingine wa eneo hilo, Benson Musungu,” Kuria alisema

Sasa uteuzi wa Mariga umesababisha tumbo joto katika chama tawala na wengi wanahoji kuwa chama hicho kifutilie mbali uteuzi huu.

View Comments