68931795_198465221148494_8284922105844220346_n

Ghost Mulee amekuwa staa wa kwanza nchini kuwakaribisha Andrew Kibe na Kamene Goro katika kampuni ya Radio Africa group. Ghost Mulee ni mtangazaji wa kituo cha Jambo kinachomilikiwa na kampuni hii.

Katika mtandao wa insta, Ghost amewakaribisha wawili hawa na kumwambia Kamene Goro ajihisi yupo nyumbani.

https://www.instagram.com/p/B2D_M-UlseX/

Redio zinazomilikiwa na kampuni ya Radio Africa Group zilikamata nafasi za kwanza mapema wiki hii na kuorodhosheshwa na utafiti wa mamlaka ya utafiti GeoPoll kama redio zinazopendwa zaidi nchini.

Soma hadithi hii:

Kampuni ya Radio Africa imeimarisha makali yake kwa kutajwa kuwa na stesheni ambazo zina wafuasi na wasikilizaji wengi humu nchini Kenya. Kulingana na matokeo yaliyotolewa na shirika la kitaifa ya Geopoll, Classic FM, Radio Jambo, na Kiss FM  ni baadhi za radio ambazo zinasikilizwa sana.

https://www.instagram.com/p/B2EAX74Frdg/

Classic FM inaongoza katika orodha hiyo ikiwa na wasikilizaji millioni 1.5 huku kipindi cha “Maina and Kingangi” kikipata nafasi ya kwanza.

Radio Jambo inachukua nafasi ya pili likiwa na wasikilizaji millioni 1.18 huku kipindi cha Patanisho inayofanikishwa na watangazaji Gidi na Ghost kikiwateka wengi sikio.

Soma hadithi hii:

Kiss FM ilijikatia tikiti ya nambari tatu ikiwa na wasikilizaji millioni 1.12 huku wasikilizaji watapata kusikia sauti geni kuanzia wiki ijayo Andrew kibe akiwa usukani akisaidiwa na Kamene Goro.

Kulingana na matokeo hayo, Radio africa kwa sasa ina asilimia 48 ya usikilizaji huku wakiwa na malengo ya kuongeza idadi ya wasikilizaji wake, hii ni baada ya Gukena fm, Smooth fm, East fm, na Homeboyz radio kujiunga na kampuni hiyo.

View Comments