Okwako alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Agnes baada ya wawili hao kutengana mwezi wa nne alipotoka nyumbani na kumuachia madeni.

Huyu bibi yangu alitoka mwezi wa nne na akaondoka lakini sijui vyema aliko. Tumekuwa tukizungumza naye kwa simu na nataka yuko kwa nani na yupo wapi.

Okwako aliongeza,

Amenifanyia makosa matatu; Ya kwanza siku moja kama fundi alisema amepata order ya kuuza vitambaa. Alipoenda nikamwambia nataka kujua dadake ili kitu kikitokea nitajua nitampigia nani.

Alirudi kwangu bila chochote na nikashindwa kwani zilienda wapi, na hilo lilitokea kwa mara ya pili na ya tatu.

Wawili wao wameoana kwa miaka 20 na wana watoto wawili, mmoja yuko kidato cha nne na mmoja yuko katika darasa la saba.

Okwako anasema kuwa ameteseka na mtoto mdogo kwani yeye hufanya kazi usiku na lazima amshughulikie mwanawe. Isitoshe jamaa anasema mkewe ana tabia za kukopa fedha mara kwa mara.

Mkewe alikopa zaidi ya kitita cha elfu 30 ambazo hamna anayejua anako peleka kwani hata ndugu zake wanasema kuwa nyumbani hamna fedha zinazowafikia.

Alipopigiwa simu bi Agnes alisema yuko Loitoktok lakini hakutaka kuzungumza hewani kabla ya kusitisha mawasiliano kati yake na mumewe.

View Comments