- samba.mapangala
- samba.mapangala.Gidi
- samba.mapangala.1

Huku bado zikiwa zimesalia siku kadhaa kabla ya mtangazaji Gidi kurejea nchini na haswa studioni, superstar huyo bado anaendelea kujivinjari huku akisherehekea siku yake ya kuzaliwa, licha kuwa siku hiyo imepita.

Gidi alitangaza kuwa mara hii, atasherehekea siku ya kuzaliwa huku akiadhimisha miaka 40, katika miji minne mikuu duniani.

Safari yake ilianzia mji wa London kabla ya kutua hadi Ufaransa alikosheherekea birthday yake na mwanawe na mkewe.

Pindi tu alipomaliza Gidi alisafiri hadi marekani anakotarajiwa kuzuru miji ya Washington DC na New York huku akikaribia kurejea nchini.

Akiwa Maryland USA, Gidi alipata bonge la surprise kutoka kwa gwiji wa Rhumba, Samba Mapangala ambaye alimuita steji na kumsheherekea mbele ya umati aliokuwa anatumbuiza.

Mapangala aliwaongoza mashabiki wake kwa kumuimbia mtangazaji huyo ambaye pia alikuwa anasheherekea birthday na gwiji anayecheza guitar katika bendi ya Mapangala.

Gidi kupitia Instagram alionesha furaha yake huku akimshukuru Mapangala.

Alisema,

The best birthday gift from veteran Rhumba Maestro Samba Mapangala here in Salisbury, Maryland USA. Thank you so much for the treat Samba. Vunja mifupa kama bado meno iko🙌.....we share a birthday with Congolese veteran base guitarist Ngouma Lukito...kwa wapenzi wa Rhumba..this is the guy who played the famous guiter in Loi song ya Koffi Olomide among many many more Rhumba songs...  am humbled 🙏🙏🙏🙏

https://www.instagram.com/p/B2Ip6RzASx3/

View Comments