- kalongo
- kalogooo
- watuu ps
- ps4 (1)
- ps123
- PS

Miaka kumi na mbili zilizopita watoto wadogo walikuwa wanajihusisha na aina ya michezo mbalimbali ikiwemo "kalongolongo", (hide and seek) ama brikicho inayvo fahamika zaidi, kuruka kamba na michezo mengine mengineyo.

Yote hayo yakiwa kabla ya mfumo wa kidigitali kuchukua usukani na kutawala maisha ya sasa.

Hivi leo watoto wa sasa hawatambui michezo hayo manake kukuja kwa tarakilishi na mashine mengine imechangia kusaulika kwa michezo za zile enzi ya nyayo.

Playstation (ps) ikiwa miongoni mwa michezo ya kisasa ambayo imenasa akili ya vijana wengi. Mchezo huu wa ps hauchezwi tu na vijana pekee, ni wazi kwamba pia wazee wamezamia mchezo huu ambao sasa umegeuka na kuwa mojawapo ya biashara ambayo mtu yeyote yule anayewekeza ndani ya biashara hii ana asilimia 75% ya kwamba atatengeneza faida kubwa.