Daaah! Malimwengu ni mengi.

Katika kipindi chetu cha Bustani la Massawe, mwanamke mmoja amefunguka na kusema kuwa ana hofu kwani amepata mimba ya jamaa mwingine ilhali ameolewa na ana watoto watatu na mume wake.

Alipoulizwa na presenta wetu wa Radio Jambo, Bi Massawe Japanni kama kitendo kicho kilitokea bahati mbaya ama kwa kusudi, amini usiamini, mama huyu alisema kuwa, haikuwa bahati mbaya na kwamba alikuwa analipiza kisasi.

Mke huyu alimpata mume wake akimdanganya na ndipo akaamua pia yeye atafanya mambo yake. Kwa sasa, mume wake anajua mtoto ni wake na hata amempa jina la baba yake. Vilevile, baba mzazi wa mtoto huyo pia anajua kuwa mama huyu amebeba ujauzito wake na kwa hivyo, jamaa huyu pia anampa binti huyu pesa kidogo za kujikimu.

Zaidi ya hayo, mwanamke huyu alifunguka na kusema kuwa, kinachompa kiwewe zaidi ni kuwa, anaona ni kama mume wake atajua ukweli kwani, mtoto ni mweupe na mume wake na yeye mwenyewe ni mweusi.

''Sasa, stress iko ni, mtoto wangu ni mweupe na bwana yangu ni mwesi. Mimi pia niko chocolate chocolate.'' alisema

Je? kilichofichika kitafichuliwa?

&feature=youtu.be