Kutana na mgombea mdogo zaidi wa ubunge wa Kibra
Dorn Anaclet, kijana ambaye ana miaka 26 akiwa mmoja wa wagombea wa kiti ya ubunge ya Kibra. Dorn anawania kiti hicho na chama cha Democratic ambacho ni cha aliyekuwa Rais wa tatu wa jamhuri ya Kenya, Mwai Kibaki.
Dorn ama "kijana mdogo" kama jina wafuasi wake wanavyopenda kumuita, ni mchanga, hajuani mtu yeyote au kuwa na 'baba wa kisiasa' tofauti na washindani wake wenye uzoefu kubwa zaidi.
Dorn huwa anafanya kampeni zake kila siku kwa miguu chini ya jua kali la Kibra akiuza manifesto yake kwa wenyeji wa mtaa huo. Yeye anapenda kuwafikia wafuasi wake kwa miguu ili kuwatambua vyema wapigaji kura, kwani huo ndio uwezo wake.
Dorn pia amewahi kuwa kiongozi katika chuo kikuu cha Nairobi huku akichaguliwa mara tatu kutumika katika vyeo tofauti ndani ya SONU.
Manifesto ya Dorn imejikita katika nguzo tatu, elimu, maji, na mazingira safi.