Mshukiwa wa kuuza bangi apigwa risasi Bungoma
Maafisa wa polisi na wale wa upelelezi huko Bungoma wamempiga risasi na kumuua mshukiwa mmoja wa kuuza bangi katika mtaa wa Moca eneo la Mandizini mjini Bungoma
Isaack Ngongu ambaye anamiaka 36 na ni baba ya watoto watatu alipigwa risasi tatu moja kuifuani na mbili shingoni na maafisa hao amabo walikuwa wakifanya msako dhidi ya washukiwa wa kuuza mihadarati inje ya nyumba yake hapo jana usiku.
Mkuu wa upeplezi kauntyi ya Bungoma amesema kwamba maafisa wake wameanzisha msako dhidi ya watu ambao wanauza madawa ya kulvta eneo hilo.
Aidha familia ya mwendazake imekashifu maauji hayo na kuomba maafisa wa IPOA Kuingilia kati na kuwapa haki kwani mwanao hakua jambazi bali alliukua tu anauza bangi.
Kwingineko, biwi la simanzi limetanda katika kijiji cha Ojame Adungos kaunti ndogo ya Teso Kusini kaunti ya Busia baada ya mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu kuangukiwa na mti na kufariki papo hapo.
-Brian Ojamaa