Samwel Kimaru ambaye ni kamanda wa trafiki, amesema kuwa karibu watu 900 wamepoteza maisha yao kutokana na ajali barabarani humu nchini.

Kimaru aliongeza kuwa ajali zimeongezeka mwaka huu ukilinganisha na mwaka jana kwa asilimia 15%.

Akizungumza huko kaunti ya Meru katika mkutano ambao ulihudhuriwa na waendeshaji boda boda, matatu, teksi, polisi wa trafiki, na maafisa wa NTSA, Kimaru alisema kuwa sheria inapaswa kufuatwa ili kupunguza ajali mingi inayoshuhudiwa humu nchini.
Vile vile aliwataka madereva wa magari inayobeba miraa kupunguza kasi wakati wanapoendesha magari hayo ili wasijihusishe na ajali ambayo inaweza kingwa kwa kufuata sheria za barabara. Aliongeza kuwa mahakama isitishe kutoa dhamana kwa watu wanaotuhumiwa kutofuata sheria za barabara.

Samuel Nyaribo ambaye ni mkufunzi wa kitaifa wa NTSA, alisema kuwa wakufunzi katika shule za kuendesha magari wanapaswa kuongeza maarifa zaidi katika sekta hiyo. akiongeza kuwa baada ya miaka miwili kila matatu litapatiwa mafunzo zaidi.

Mwenyekiti wa matatu eneo la Meru Raymond Ikiara alisema elimu ya barabarani ni nzuri na kila matatu inapaswa kuikumbatia.