ayako

Cecilia Kwamboka Ayako, mwanafunzi katika shule ya upili ya Musa Nyandusi atakuwa anatarajiwa kufanya mtihani wa KCSE mwaka huu. Mwanafunzi huyo ambaye ako na miaka 32 tayari ako na watoto wawili kutoka kwa ndoa ambayo ilisambaratika.

Gazeti la The Star ilipatana na yeye jana katika shule yake, huku akionyesha ujasiri akijitayarisha kuukalia mtihani huo.

Kwamboka alilazimika kurudi shuleni baada ya umasikini kukithiri na ndoa yake kusambaratika. Kwamboka alieleza kuwa yote hayo yalianza wakati alienda kutafuta kazi na mwajiri akamuitisha cheti cha kuhitimu kidato cha nne ambacho hakuwa nacho.

Kwamboka aliolewa akiwa kidato cha tatu hivo basi hakukamilisha masomo yake na muda uliposonga mumuwe alianza kumdhulumu na kumtusi huku akiwaleta wanawake wengine nyumbani kwao.

Ni tukio ambalo ilimghadhabisha Kwamboka kiasi cha kwamba kidogo awatendee mabaya mumewe na wanawake wake lakini aliamua kurudi nyumbani kwa wazazi wake. Wakati huo, Kwamboka aliamua kurudi shuleni kumaliza masomo huku wasiwasi yake ikiwa ni kupata fedha ya kumlipia karo.

Kwamboka alielezea The Star kuwa kwa bahati nzuri alikutana na mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Kisii Janet Ongera ambaye alijitolea kufadhili masomo yake jambo ambalo alimshukuru sana.
Kwamboka alisema kuwa atajitahidi kufaulu katika masomo yake ili aweze kuanzisha shirika la kupigania haki za wanawake katika mkoa huo.

Aidha Kwamboka alieleza kuwa anapitia changamoto haba kwani inampasa aondoke shuleni mapema ili kuwashughulikia watoto wake ambao wako darasa la 5 na 6 lakini hiyo haitamfanya afe moyo.

Mwakilishi wa wanawake kaunti ya Kisii Janet Ongera alisema kuwa wanawake wengi wamepoteza mwelekeo baada ya kujihusisha na ndoa za mapema.