unnamed__1___1568616791_28847

Hali tete na utovu wa usalama ilishuhudiwa katika kanisa la AIPCA Nanyuki jana.

Hii ni baada ya wafuasi wa mwakilishi wodi kaunti ya Laikipia Catherine Waruguru kuvamia kanisa hilo.

Mbunge mteule Maina kamanda alikuwa akihutubia waumini kuhusu mapendekezo ya BBI na Punguza Mzigo wakati huo.

Soma hadithi nyingine:

Ilimlazimu Askofu Ndirangu Ngunjiri amwamrishe Waruguru kutoka nje kwa misingi ya hakuwa amealikwa katika ibada hiyo.

“Nimepokea habari za kijasusi kwamba Waruguru ataingia humu bila ruksa kwa hivyo nikafahamisha Kamanda atoke kupitia mlango tofauti atakapoingia. hakuwa amealikwa na lengo kuu ni kuleta zogo." Alisema Ngunjiri

Ngunjiri ametoa taarifa kuwa Waruguru aliwasili na kundi la wafuasi 200 waliokuwa walevi hivyo akanyimwa fursa ya kuongea na waumini.

Waruguru alikusanya wafuasi wake katika kiwanja cha Thingithu na kutoa kauli za kumkashifu Kamanda.

Aliyekuwa mwakilishi wodi mteule kaunti ya Laikipia amedokeza kuwa Waruguru anatumika katika vuguvugu za kushinikiza juhudi za kumchagua Ruto mwaka wa 2022.

"Tunataka kumwambia Askofu Ndirangu kuwa asisahau kuwa alikuwa anapika kiamshakinywa kwa Ruto Karen anapotembelewa na viongozi wa kanisa. Atangaze msimamo wake wa kisiasa anaofuata." Waruguru.

Soma hadithi nyingine:

Waruguru alitangaza kuwa anawaza kugombea kiti cha Laikipia 2022.

“Nitagombea kiti hicho...na najua watu watanichagua. Ila kwanza tuangalie kadi ya uchapakazi..." Alisema Waruguru.

Askofu Ngunjiri alisema kwamba alimfukuza Waruguru kwa sababu alikuwa amealika Kamanda, rafiki yake, na kuwa kanisa la sehemu ya kufanyia siasa.

"Kamanda atakuwa hapa Oktoba 13 katika harakati za kutayarisha mapokezi ya rais Kenyatta. Waruguru aombe msamaha kutoka kwa mungu kwa kudhubutu kuvuruga ibada..." Askofu Ngunjiri.

View Comments