- rashid
- loulou

Watangazaji stadi, Lulu Hassan na Abdalla Rashid wa Citezen Tv hufanya kazi pamoja, wakati mmoja na wengi hupendezwa na uzuri wao.

Wapenzi hawa wamebarikiwa na watoto watatu, vijana wawili na binti mmoja.

Kidosho Lulu alipoulizwa kama huwa wanakosana, Lulu alijibu na kusema kuwa huwa hawakosani mara kwa mara.

''Mwathakui: Beautiful couple. Sasa nyinyo hukosana???Asking for a friend.

 Lulu naye akajibu,

           ''LOL. SIO SANAAA.''
Mwingine naye alimuuliza Lulu huwa anajiskia vipi akifanya kazi na mume wake

Shabiki mwingine naye alimuuliza '' How does it feel to work with your hubby at the same place..to me it’s kinda difficult.''

''IMAGINE ITS FUN. WE GET TO SPEND A LOT OF TIME TOGETHER.'' Lulu alisema.

Tazama Orodha ya maoni za mashabiki kwenye mtandao wa kijamii,

Zaidi ya hayo, katika mahojiano ya kale kidogo ya Rashid, alifunguika na kusema kuwa, mpenzi wake Lulu alibadilisha maisha yake.

''ALINIBADILISHA MAISHA YANGU, MIMI NILIKUA MTUKUTU SANA…MIMI NILIPENDA SAUTI KABLA YA KUONA SURA. NIKASIKIA SAUTI…ILE SAUTI ILIKATA KAMA KISU KWENYE MOYO WANGU…SIKUJUA NI YA NANI LAKINI NIKAMWAMBIA YULE JAMAA ALIYEKUA ANANIFANYIA INTERVIEW HII SAUTI, HUYU MSICHANA ANAONEKANA NI MZURI..SAUTI ILIENDA SAMBAMBA NA SURA NA TABIA NA KILA KITU KWA HIYO SIJUTII.''

Vilevile, katika sherehe ya kuzaliwa ya Lulu Hassan, mume wake Rashid aliamuandikia ujumbe ufuatao;

''Ukiniuliza @loulou_hassan ni nani kwangu daima upata ugumu kutoa jawabu kwa sababu yeye ni zaidi ya kila jibu langu. Mpenzi mzuri ni anayefahamu mapungu na udhaifu wako kabla kuzingatia ubora wako. Hakuna zaidi ya asante kwa Maulana pamoja na kumuomba atujalie baraka tele na maelewano 2017. Zile fitina na changamoto tuendelee kuziangalia kitoto. Mola akutangulie daima @loulou_hassan . Kwa wale “wapenzi watazamaji” asanteni kwa kumtizama kwani nyinyi ndio yeye lakini MIMI ndiyo YEYE Lol . Kila jema tunapoanza 2017. Wewe ndio mwaka wangu @loulou_hassan na hii 2017 itakosa maana bila uwepo wako maishani mwangu. Mungu atulinde sote.''

Ama kwa hakika, mapenzi ni matamu.