- kambua.hubby
- gospel
- Kambua-Cover-300x185

Kambua Manundu si mwanamziki wa nyimbo za injili pekee yake bali pia ni mke wa bwana  mmoja na mama wa mtoto mmoja.

Vilevile, Kambua anapenda sana muziki na ni dhahiri kwani binti huyu ana mziki freshi sana.

Familia ya Kambua

Kambua ni mtoto wa pili kwa familia ya watoto watatu na wazazi wawili, Profesa Manundu na Mweneza injili Bi Lois Manundu ambao ni waanzilishi wa Tabibu Ministries.

Maisha ya mwanzoni ya Kambua.

Kambua alikuwa binti ambaye alipenda sana michezo ya kivulana na mara kwa mara,alikuwa akicheza na ndugu zake wa kiume.

Kidosho huyu alienda shule ya msingi ya Kianda na hapo ndipo imani yake ilikuzwa kwani alikuwa anashiriki sana kwenye mambo ya kwaya na ibada za misa.

Kambua alienda kwenye shule ya upili ya Lukenya ambapo upendo wake wa muziki uliongezeka na akaanza kuimba nyimbo zake mwenyewe.

Pasi na kupata shida ya kulipa karo, alijaliwa na Maulana kwani alipata bahati na kumaliza masomo ya shule yake ya upili na kupata bahati ya kuenda kusomea sanaa ya muziki  ng'ambo kwenye chuo kikuu cha Ambrose kilichopo Calgary.

Hata hivyo, kabla ya kuenda Ng'ambo, Kambua alitoa nyimbo na mastaa kama Mbuvi, Bahati na Kavutha.

Alipomaliza digrii ya muziki ng'ambo, Kambua alikuja kenya na kushuhudia vile ambavyo wimbo wake 'Nishikilie' ulikuwa unavuma na hapo ndipo akaamua kuwa atabaki mumu humu nchini na kuendeleza sanaa yake.

Zawadi ambazo Kambua amepata.

Mwaka wa 2008, Kambua aliteuliwa kuwa mwanamke bora katika tuzo za Kisima.

Mwaka wa 2009 akashinda Groove Awards.

Ushindi huu ulimsaidia sana kupata kazi ya kusherehesha katika hafla na kuwa mtangazaji wa vipindi kama Bambika.

Ndoa ya Kambua

Kambua na mpenzi wake bwana Jackson Mathu walifunga ndoa za maisha katika Hoteli ya  Windsor Golf mwaka wa 2012.

Kwa sasa wamebarikiwa na mtoto mmoja wa kiume.

Mbali na hayo, Kambua alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mbuvi lakini wakakata uhusiano wao na mwanamziki huyu kwa sababu tusizozijua.

Vilevile, Kambua anapenda viatu na kofia sana na ni wazi kuwa ata anavyo vaa, tunaweza kujua kuwa binti huyu anajua kuvaa si kidogo.