Hivi leo kwenye kipindi chetu cha patanisho, Binti mmoja, jina lake Irene Atieno alipigia Gidi na Ghost na kuomba Radio Jambo impatanishe na mume wake waliokosana kwa sababu ya pesa na sababu nyingi ambazo hakuzisema.

''Kulikuwa na sababu nyingi zenye zilifanya tukosane na mume wangu lakini sanasana ilikuwa hii ya pesa'' Irene alisema.

Irene alisema kuwa, mume wake na yeye walikosana baada ya dada yake kumwibia  mume wake pesa zilizokuwa kwenye akaunti ya benki  shilingi 33,500 Irene alikuwa anaishi na mume wake mpaka siku moja ambayo mume wake alikusanya virago vyake na kuhama nyumba bila kumwambia mke wake anapokwenda na kumwachia watoto wote.

Binti huyu alijaribu kumwomba mume wake msamaha lakini maombi yake yote,yaliambulia patupu.

Zaidi ya hayo, watoto wa mume huyu walienda kumsalimia baba yao na walipoenda, walipata mwanamke mwingine huko na baba yao kitu ambacho ni wazi bayana kuwa, baba yao alioa mke mwingine na ndio sababu hataki kujihusisha na Bi Irene na watoto wake.

Vilevile, Bi Irene alisema kuwa, hata kama mume wake ameoa, hana shida kuishi na mume wake kwani, anataka walee watoto wao pamoja na mume wake.

''Nataka kama inawezekana, turudiane na mume wangu kwa sababu ata watoto wananiuliza kwani baba alienda wapi?'' Irene alisema.

Mume wake alipopigiwa simu, Bi Irene alijaribu kumwomba msamaha lakini akasema kuwa hataki kufanya kitu chochote na Irene na papo hapo, na baada ya dakika chache, akakata simu yake.

Si tulishamalizana mbona tena unanipigia simu? Msamaha msamaha inanisaidia na nini?

Je? tutamsaidia aje Irene?

View Comments