jchmytqjmfwjan5b583482446bb

Staa na nyota wa Bongo Rich Mavoko sasa anasema kuwa hana damu ya ubifu na lebo ya WCB.

Rich amefunguka mwanzo mwisho kuhusu kilichopelekea yeye kuitema lebo hii.

Akizungumza na chombo cha habari nchini humo, Rich ameweka wazi uhusiano wake sasa na WCB.

Tamko la Rich linajiri punde tu baada ya Mwarabu Fighter kuibua masaibu aliyoyapitia kipindi alipokuwa mlinzi wa Diamond Platnumz.

Soma hadithi nyingine:

Alipoulizwa kuwa iwapo sasa ana uadui na Diamond Platnumz, Mavoko alisimulia,

"Hamna uadui kiukweli. Unajua siwezi kuingia kwenye moyo wa mtu au kichwa chake ili nijue anawaza nini lakini kwangu mimi hamna uadui."

Rich anasema biashara yake usafini aliifunga na kuomba ruksa ya kutoka,

"Kwa sababu mimi naamini ni biashara imeshakwisha hatuna haja ya kutaka kuweka chochote tukiweka tutaonekana kama watoto..."

Soma hadithi nyingine:

Mavoko anasema mkataba wake na lebo ya Wasafi ilikuwa ya hiari na kwa hivyo kuufunga sio tabu,

"Sitaki kuongelea tena sababu lakini nashukuru mungu vitu vinakwenda tena vinaisha lakini mimi nasema ni biashara ilifikia pale ikabidi iishe hatukuwa na ulazima."

"Biashara ni vitu za hiari mimi naweka talent wewe una-invest so ikifika kipindi sielewi tunaweza tukaongea tukamaliza kulikuwa hakuna ubaya wowote."

Ila ni kitu haswa kilimtoa staa huyu katika lebo kubwa Afrika mashariki?

"Kuna vitu ambavyo niliona vinaenda kinyume na vile nilikuwa nataka na mimi pia napenda kujipima."

Soma hadithi nyingine:

Mamake Rich alikuwa mtu wa kwanza kuhusu kazi ya mtoto wake,

"Hata mama pia alikuwa ananiambia nijifunze kujipima maana kuna vitu vingi vilikuwa vinapungua kwangu."

"Kwa kukaa muda mrefu jikoni halafu bila kutoa mapishi ambayo uko nayo."

"Nilikuwa narekodi material mazuri halafu yapo tu ndani nikiuliza kuhusu label inakuwa ni mambo ya kukimbiana kimbiana."

Soma hadithi nyingine:

"Kuna kipindi nilikaa muda mrefu bila kutoa kazi hadi Mamangu mzazi akawa amepanic, ikabidii awapigie simu wahusika, maana alikuwa ananiambia kuwa kila siku narekodi lakini kazi hazitoki kwa hiyo nitaishia kuwa chizi muziki."

"Yaani nikiwa pale sikuwa naona future yangu. Kila siku imekuwa ni kuzungushana. So mimi nikaona isiwe tabu hii ni biashara na hatugombani nikaona wacha na mimi ni move lakini ikawa ngumu kidogo kwa kuwa wenzangu hawakunielewa kwa haraka haraka."

"So nikaona isiwe tabu nikwaambia naomba kuondoka, ili nifanye vitu vyangu," Akamalizia Rich Mavoko.

View Comments