bangi

Matumizi ya bangi kama kiburudisho miongoni mwa vijana umeongezeka, huku matumizi ya miraa na shisha ukiwa umedidimia kulingana na uchunguzi mpya uliofanyika.

Matumizi ya sigara ulikuwa asilimia tatu ukiwa bado unashuka. Utafiti ambayo unafahamika kama Holla, ulitolewa na kampuni ya Consumer Insight siku ya alhamisi katika ofisi ya Riara, jijini Nairobi.

Vijana wapatao 1,634 walio na umri kati ya 13-30, walifanyiwa uchunguzi katika kaunti 16 kati ya januari na machi mwaka huu wakiwakilisha asilimia 50% ya wakazi wa Kenya.

Asilimia 8 ya vijana hao, ulibainika kuwa walikuwa wanatumia miraa, bangi, na shisha kama burudani. Hata hivyo matumizi ya miraa na shisha ilikuwa inapungua huku utumiaji wa bangi ukiongezeka.

Shisha ambayo ulipigwa marufuku kutumiwa humu nchini na wizara ya afya mnamo mwaka wa 2017, kwa sasa hairuhusiwa kutumika mikahawani, vilabuni vya pombe, ama mahali popote pale. Kufuatia marufuku hiyo, Kenya sasa ni nchi ya tatu humu afrika mashariki baada ya Tanzania na Rwanda kupiga marufuku utumizi wa bidhaa hilo.

Asilimia 17% ya vijana ambao wako kati ya umri 13-30 wanatumia pombe. Lakini matumizi yake ikiwa inashuka huku bidhaa zinazopendwa zaidi zikiwa Tusker, Guiness, Kenya cane, Jameson, Smirnoff Ice, Amarula, Fourth Street, na Caprice.

Ripoti hiyo ilionyesha zaidi kuwa asilimia 5% ya vijana walichukulia kamari kama kazi. Asilimia 38% ya wanaume walijihusisha na michezo ya kamari mwaka jana huku asilimia 8% ya wanawake walishiriki katika mchezo huo wa kamari.

Vijana asilimia 28% kutoka hali duni ya uchumi walicheza sana kamari, huku watu wa daraja la kati na juu kimaisha wakiwa na asilimia 22% ya kujihusisha na mchezo wa kamari.

Katika matumizi ya mipango ya uzazi, asilimia 28% wamewahi tumia kondomu, huku asilimia 16% wakitumia sasa.

Asilimia 26% wamewahi kutumia sindano ukilinganishwa na watumiaji wa sasa wenye asilimia 16%

Asilimia 23% wametumia tembe za kupanga uzazi ukilinganisha na asilimia 10% wanaotumia sasa.

Hofu ya kifo vile vile umebainika tishio miongoni mwa vijana, ukichukua asilimia 51% , ukimwi ukifuata na asilimia 39%, na magonjwa mengine yakichukua asilimia 39%