WhatsAPP
Mswada mpya wa kudhibiti mitandao za kijamii  unatarajiwa kuwasilishwa Bungeni juma hili.
Kwa mujibu wa sheria za maguezi ya mawasiliano, mswada huu unalenga kuwashinikiza wasimamizi wa makundi ya WhatsApp na Facebook kuchukua leseni kutoka serikali kabla ya kuyafungua makundi hayo.
Hivyo basi kabla ya kupewa leseni hiyo utahitajika kutozwa ada kama malipo ya kuidhinishwa.
Mswada huu ambao uliwasilishwa na Mbunge wa Malava, Malulu Injendi itakuwa ni kinyume na sheria kufungua kundi lolote katika Facebook au WhatsApp bila kupata idhini kukoka mamlaka ya mawasiliano nchini.
Aidha, wasimamizi wa vikundi hivyo watawajibikia kwa jumbe zote ambazo zitakuwa zikisambazwa mitandaoni. Na wale watakaokiuka sheria hiyo watahukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezni, faini isiyozidi Sh 200, 000 au adhabu zote mbili.
Kulingana na mswada huu, wasimamizi wa vikundi hivyo vya kijamii wanapaswa kuwa na majina kamili ya wanachama wao pamoja na maelezo zaidi kuhusu wanapoishi. Isitoshe, wanatakiwa kuwajibikia ujumbe zote zinazosambazwa kwenye makundi yao na kuwaondoa wanachama wanaotuma ujumbe zisizofaa.
Watajukumiwa kuhakikisha kwamba wanachama wake wamefikisha  umri wa miaka 18 na zaidi.
Iwapo mswada huu utapitishiwa Bungeni, mablogu watatakiwa pia kupata idhini kutoka kwa serikali kabla ya kuendesha shughuli zao.
Mswada huu unalenga pia wale wanaochapisha makala mitandaoni, wanaohakiki na wasambazaji ujumbe.
Hata hivyo Kamati ya Bunge ya Teknolojia Habari na  Mawasiliano ikiongozwa na mwenye kiti William Kisang, anasema kwamba itakuwa vigumu kudhibiti mamilioni ya watumizi ya mitandao ya kijamii.
 Kisang anasema kwamba kile Mamlaka ya Mawasiliano kinachocharibu kudhibiti tayari kimeshughulikiwa na  sheria iliyopitishwa mwaka uliopita. Sheri hiyo inahusu Matumizi mabaya ya Kompyuta  na Uhalfiu wa Kimitandao.