24__1569485929_41121

Siku chache baada ya staa na nyota wa Bongo Diamond Platinumz kutoa usemi kuwa Harmonize alimsaliti kwa kuitema WCB, mkali huyu sasa amezidisha walinzi wake hadi kufikia 10 na ushei.

Kitendo cha Diamond kuwa na walinzi wengi ni kero kwa Harmonize ambaye ubuyu Bongo unasema kuwa anashindana na bosi wake kwa walinzi.

Haya yalitokea jana wakati Mondi alikuwa ameita kikao na wanahabari kusaini dili nono ya Sabuni ya Nice One.

Soma hadithi nyingine:

https://www.instagram.com/p/B21lKX5HgNy/

"Tunahitaji sabuni ambayo hata ufulie kwa maji ya chumvi itakupa matokeo ni Nice." Alisema Mondi

"Yaani ni kitu nilikuwa natamani niwe balozi wa kitu kizuri." Alisema Mondi.

Kupitia kipande cha video Insta, ni kweli kuwa kitendo cha Konde Boy kuitema lebo kilimuuma.
Soma hadithi nyingine:

“Raisi pekee ambaye wananchi wamemchagua, nishasalitiwa na JESHI ila wakashindwa kunipindua” Diamond alisema.

Ubabe wa walinzi sasa unaonekana ndo mtindo mpya Tanzania.