uturuki

Kwa siku chache sasa, mtangazaji Massawe Japanni amekuwa 'Akila life na adabu'. Nikisema hili namaanisha kuwa amekuwa akijiburudisha huku wengi wetu tukiwa kazini.

Massawe aliondoka wiki iliyopita na kusafiri hadi Uturuki kwa likizo ya siku kadhaa baada ya miezi ya kuwaburudisha mashabiki wake hewani, katika kipindi cha bustani la Massawe.

Kupitia Instagram, mtangazaji huyu mama wa watoto watatu, alichapisha picha kadhaa akiwa safarani na pindi tu mashabiki walitaka kujua aliko, aliwajulisha kuwa alikuwa safarini akielekea Dubai.

Isitoshe, alimwambia shabiki mmoja kuwa wiki hii yote hatokuwa hewani kwa kipindi chake ambacho huja kuanzia mida ya saa nne asubuhi, kwani bado hatokuwa amerudi.

Hata hivyo, Massawe sasa yumo Uturuki ambako amekuwa kwa siku kadhaa na akiwa humo, jambo moja ambalo amejifunza ni kuwa madereva nchini humo ndio wasiojali, ikilinganishwa na wengine duniani.

Massawe alisema haya kupitia mtandao wa Instagram alipochapisha picha yake akiwa kando ya barabara moja nchini humo akidai kuwa amejifunza kuwa makini kila anapovuka barabara.

Alisema,

Every coin has two sides, just like most people have two faces...Stay Woke!! Wacha sasa nivuke Barabara, Turkey drivers are the most reckless drivers in the world...If I'm posting sikugongwa🤣🤣 🇰🇪🇹🇷

Tazama picha za mtangazaji huyu akiwa Uturuki,

https://www.instagram.com/p/B2zcw84BxS2/

https://www.instagram.com/p/B21PX0ZAmol/

https://www.instagram.com/p/B23KJaSAQmy/

View Comments