Hivi leo Katika kipindi chetu cha Patanisho Bwana mmoja alituma ujumbe na kusema kuwa anaomba apatanishwe na mke wake kwani hawaelewani nyumbani.

Alipoulizwa na  Gidi sababu ya kutoaminiwa alisema kuwa, mke wake anamshuku ana wanawake wengi kwa sababu amempata akizungumza na wanawake wengi mara kwa mara.

Bwana huyu jina lake Edwin alijitetea na kusema kuwa mabinti wale ni rafiki zake waliosoma pamoja na mambo wanayoyazungumzia ni ya kale.

''Sisi huwa tunaongea story za shule tu.'' Edwin alisema.

Hata hivyo, mke wake haamini anachoambiwa.

Cha kusikitisha ni kuwa, mke wake Edwin alipopigiwa, hakutaka kuzungumza kwani, aliposhika simu yake, hakusema lolote.

Licha ya hayo, Edwin alimhakikishia  mkewe kuwa hana mpango wa kando na kumwomba mke wake awache kumshuku .

Je kitendawili hiki cha wapenzi hawa kitateguliwa?

View Comments