crime

Kweli mapenzi yana taabu. Eunice Njeri ni binti ambaye alihukumiwa kifungo kwa sababu ya wizi wa mabavu.

Eunice alipofika mahakamani siku ya kesi kusikizwa, alifunguka na kusimulia kisa chake ili aweze kujiokoa.

Akiwa na simanzi na majonzi, binti Eunice alisema kuwa, aliyekuwa mpenzi wake wa kitambo  ndiye alimbandika makosa tele ya wizi wa mabavu na kuhakikisha kuwa amefungwa kwa sababu ya kukataa kuwa mpenzi wake tena.

Eunice alisema kuwa, kisa chake cha mapenzi na jamaa huyu kilikuja kuwa kisa cha mapenzi ya uchungu sana kwani afisa huyu wa polisi alimhukumu kwa sababu ya kukataa mapenzi yake.

“This is a love story that turned sour. I am innocent and this case is some sort of punishment for refusing to take back my ex-lover, the arresting officer,” Eunice alisema.

Njeri aliambia korti kuwa, anakazana na kesi ambayo ilisababishwa na mapenzi yaliyoisha kitambo sana.

Njeri alimwambia Barbara OJoo hakimu mkuu wa Kibera kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na afisa Mohammed kwa muda mrefu kabla ya kukata kauli kutengana,.

Zaidi ya hayo, binti huyu alisema kuwa afisa huyu wa polisi alijaribu mara kwa mara kuwa na uhisiano wa mapenzi naye lakini akakataa kwa sababu tabia zake hazikuwa zinampendeza  na ndipo asifa huyu akaapa kumpa funzo kali.

''He tried several times to get me back but I could not do that because of his behaviour which I could not stand. He swore to teach me a lesson,'' aliambia korti.

Alisema pia Mohammed alimpata Kangemi mjini Nairobi ,akamshika na kumwingiza kwenye gari la polisi alilokuwa akiendesha kisha akampeleka kwenye kituo cha polisi.

Njeri alisema kuwa afisa huyu wa polisi alimzungusha mtaa wa Loresho huku akijaribu kumsisitizia amrudie.

"I was driven by Moha in a police vehicle urging me to love him. Sometimes he used persuasion and when it wasn’t bearing any fruit, he would use threats such as saying he would make life very difficult for me," alisema.

Zaidi ya hayo, afisa huyu alimfungia binti huyu, pamoja na mtoto wake mchanga kwenye seli ya Kabete na kuenda zake.

Vilevile, Eunice alifunguka na kusema kuwa, alisaidiwa na binti mmoja ambaye alimpa simu yake apigie mama yake ambaye baadaye alikuja na kumchukua mtoto huyo.

"I was saved by a female detective who gave me her mobile phone to call my mother who later came and picked my child," alisema.

Njeri alisema kuwa, Mohamed aliporudi na kumpata hana mtoto, alimuita kahaba na kusema kuwa aliwasuta maafisa wa polisi na kumwambia amsaidie.

Licha ya hayo, Eunice alisema kuwa, Mohammed alirudi kama amekasirika sana na kumwambia aweke sahihi na kuchukua alama ya vidole na baaada ya dakika chache akajipata amehukumiwa kwa kosa hili la wizi.

“He sounded so angry. He brought some papers which he forced me to sign and took my fingerprints. The next thing I knew, I had been charged with this offence,” Eunice alisema.

Katika rekodi za Polisi, Njeri alishtakiwa kwa kumwibia bwana Thomas Mwavali bidhaa za electroniki zilizo gharimu shillingi 112, 000.

Mshtaki alisema kuwa, Njeri pamoja na wenzake ambao hawako kortini walimgonga Mwavali kabla ya kumwibia.

Mwavali aliwaambia polisi kuwa alikuwa ametoka kwenye klabu pale alikuwa ametoka kutizama soka, saa 1.30 asubuhi na kupitia njia fupi ili afike nyumbani haraka.

Mwavali Alipofika nyumbani kwake, mtu mmoja alimvuta na wengine wakamgonga na papo hapo akapoteza fahamu.

“When I reached my house, someone pulled me from behind and others grabbed me, then they hit me with an iron bar. I blacked out but could hear a lady’s voice,” Mwavali alisema.

Vilevile Mwavali alisema kuwa, wezi wale walifungua mlango  wa nyumba yake kwa nguvu na binti yule pamoja na wenzake wakaanza kubeba vitu.

Ama kwa hakika mapenzi yana mambo.

View Comments