Wakenya hawakurudisha shilingi bilioni Sh7.38 ambazo sasa hazina maana wala dhamana, gavana wa CBK Patrick Njoroge ametangaza.

Akizungumza katika kikao na wanahabari siku ya Jumatano, Njoroge alisema kuwa kati ya noti milioni 217  za elfu moja, ni milioni 209.6 million pekee ambazo zilirudishwa kabla ya kipindi kilichotengwa kukamilika.

"Ilipofika Septemba 30, noti 209,661,000 ndizo zilikuwa zimebadilishwa na hiyo inamaanisha kuwa noti milioni 7,386,000 bado zipo mikononi mwa watu," Njoroge alisema.

Aliongeza, "The hypothesis that Kenyans are procrastinators and wait until the last minute was disproved. Kenyans will act properly when they know what is good for them."

Njoroge aliongeza kuwa walifanikiwa na shughuli ya kubadilisha sarafu hizo huku akiongeza kuwa , kitengo cha kupambana na uporaji wa fedha na kupambana na ugaidi kikiwa tayari kupambana na kila kitu.

Alisema kuwa mipango yao ilizuia fedha ambazo wenyewe hawakutaka zipigwe msasa kikamilifu. Gavana huyo wa benki kuu ya Kenya pia alielezea njia waliochukua ili kuangamiza noti hizo mzee.

Alisema kuwa ukiweka noti hizo milioni 217, zinaweza toshea kwenye magari matano tu aina ya trela.

"When we receive banknotes, we punch them and shred them, then compact them into a briquette. Each briquette the Governor is holding is equivalent to Ksh 1,000,000 in shredded banknotes," Njoroge alisema.

Alisema kuwa shughuli 3,172 za tuhuma zilitambulika katika kipindi hicho cha kubadilisha sarafu.

"The volume of total transactions just in August alone was 161,082,470, to give a sense of scale," Njoroge alielezea.