Leo kwenye kitengo cha patanisho kwenye Gidi na Ghost asubuhi, Mwanamke mmoja jina lake Mary alifunguka na kwa huzuni akasimulia vile mumewe alimfanyia.
Mary alisema kuwa anashangaa ni vipi mume wake, atakuwa na mpango wa kando na ilhali  wameishi katika ndoa kwa miaka 37.

Amini usiamini, mume wake Mary, jina lake Caleb alishiriki ngono na mrembo wa umri mdogo  kulingana na miaka ya Caleb.

Caleb mwenye umri wa miaka 57 alikuwa na  uhusiano na binti mwenye umri wa miaka 28 kwa muda wa miaka miwili.

Mary alisimulia kisa chake na kusema kuwa, yeye na mume wake huwa hawaishi pamoja na wakati ulifika ambapo alikuwa anaona tabia za mumewe zimebadilika.

Mary aliamua kuomba Mungu ambadilishe mume wake lakini bado hakuacha hulka zake za kuchovya nje.

Wakati moja mambo chombo kilipoenda mrama kabisa, Mary aliamua Kuwatuma watoto wake wawili mjini Eldoret kutembelea baba yao.

Watoto walipofika kwa nyumba ya baba yao, walishikwa na butwa kupata nguo na bidhaa nyingi za mwanamke mwingine na kumjulisha  mama yao.

Gidi alipigia simu na kumuuliza Caleb mbona alienda nje ya ndoa na akashindwa kujitetea.

''Aki mimi sikujua ni nini ilikuwa inanifanya nifanye hivyo, lakini si unajua hii kitu hainanga macho.'' Caleb alisema.

Baada ya mazungumzo mafupi, Caleb alikula kiapo na kusema kuwa hatarudia kosa lile na kukiri kumkosea mkewe.

Mary alifurahishwa sana na maneno matamu yaliokuwa yakitoka kinywani mwa mumewe, na kumsamehe. Alimwahidi kumpakulia chumbani walivyokuwa wakifanya wakiwa baru baru.

''Mimi nakupenda sana Caleb na leo ujitayarishe. Nitakupea kitu yako vizuri kama kawaida. Leo kutakuwa kumoto kama  venye kulikuwa siku ya harusi yetu.''Mary alisema.

Ama kwa hakika, ni bayana kuwa, mapenzi hayachagaui umri.