unnamed (9)

Nembo mpya itakuwa na herufi tano za  jina la kwanza la Kipchoge, "Eliud" na nambari "1:59" kuashiria shindano hilo.

Safaricom imebadilisha nembo yao ya M-Pesa kwa siku saba zijazo kama njia ya kuonyesha uaminifu wao  na kumpa motisha  bingwa wa dunia katika mbio za masafa marefu Eliud Kipchoge.

https://twitter.com/SafaricomPLC/status/1181851592296976384?s=20

"Ni heshima kubwa kwa Safaricom kuhusishwa na huyu mtu wa maana Eliud Kipchoge" kaimu mkurugenzi mtendaji Michael Joseph alisema Jumatano.

"Ni adhama na tunu kubwa kwetu kwa kupata fursa ya kumkabidhi nembo yetu ya M-PESA  kwa bingwa huyu anayefaa," alisema.

Joseph alisema ni mashindano bora ya kibinadamu ambayo huhitaji talanta na juhudi madhubuti ili kufanikisha.

"Katika suala hili, tutaenda zaidi na tutamfanya Kipchoge kuwa balozi wetu; Kwa usawa, Safaricom pia itakuwa balozi wa Eliud Kipchoge," alisema.

View Comments