unnamed (2)-compressed

Nguvu za mapepo zimeshindwa baada ya daraja kujengwa katika Mto Mkuu ambao unaaminika kuwa na majini hatari wanaosababisha maafa wakati wa mafuriko.

Wakazi wanasema waganga wamekuwa wakitumia nguvu zao kuhakikisha kuwa daraja halitajengwa.

Lakini uchawi wao umeshindwa baada ya serikali kuahidi kuwa daraja litajengwa.

Waganga wanasemekana kufanyia matambiko yao katika mto huo.

Siku ya Jumatatu mbunge wa Kilifi Kusini Ken Chonga aliweka jiwe la msingi la Daraja la shilingi milioni 5 kwenye Mto Mkuu linalounganisha divisheni za Chony na Mtwapa. Ujenzi unatarajiwa kuchukua miezi 10.

Daraja litajengwa kwa kima cha Shilingi milioni 56 na linatarajiwa kukamilika kwa kipindi cha miezi 10.

Mwaka jana watu wanne walisombwa na mafuriko katika mto huo.

Kabla ya jiwe hilo la msingi kuwekwa, ibada ya kanisa ilifanyika kutoa pepo kutoka kwenye mto huo amabo umewaponyoka wakaazi watu wanne katika kipindi cha miaka miwili.

Akiongea wakati wa kutia jiwe la msingi, Chonga alisema Daraja hilo lilifaa kujengwa kitambo sana kwa kuwa mto huo umekuwa chanzo cha maafa mengi sana.

"Daraja hili ni muhimu, hususan kwa uchumi. Chonyi hutoa mazao mengi ya kilimo na soko kuu ni Mtwapa. Njia fupi ya kwenda sokoni ni kuvuka mto huu. Wakati mvua inanyesha huwezi kuvuka kwa sababu mto umejaa, ”Chonga alisema.

Alisema madereva wa boda boda ambao huvusha watu kwa huo mto wamevamiwa na kubibiwa na wakora.

Kuna sehemu ambayo watu huvuka wakati maji yanapungua. Ni mwinuko sana na majambazi hungojea mara kwa mara wanunuzi hao na kuwaibia.

Wanafunzi katika shule za karibu za Tunzanani na Kidutani hawawezi kwenda shuleni au kurudi nyumbani wakati kunanyesha na mto umejaa.

"Unaweza kuvuka na ghafla unapatwa na mafuriko ilhali hakujanyesha seheemu hiyo.' alisema.

Njia hiyo pia ni njia ya watu wanaoelekea Nairobi kutoka Mtwapa ambao hawataki kupitia Mombasa.

Mbunge huyo alisema kuna mipango ya kuweka lami hiyo barabara ili kuunganisha Mtwapa na barabara kuu ya Mavueni Mariakani kupitia Chasimba.

Mfanyabiashara Amina Ali alisema daraja hilo litawawezesha kufanya biashara bila woga.

View Comments