patanisho

Jennifer alituma ujumbe akiomba ndoa yake na mumewe bwana Aggrey iokolewe.

"Kuanzia mwaka Jana mwezi wa tisa mume wangu ambaye hufanya kazi karibu nami na alianza kukosa Kuja nyumbani na kila nikimuuliza anasema hana fare. Sasa nikimtumia fare yeye akija nyumbani utaona hana haja hana shughuli na tabia zimebadilika." Alijieleza Jennifer.

Aliongeza,

Nataka tu aniambie nilikosea wapi ili nirekebishe kwani hajawahi niambia lilote.

Wawili hawa wamekuwa kaa ndoa ya miaka 12.

Alipoulizwa mbona hajawahi wasilisha kesi yake kwa familia ya mume wake alisema,

Unajua watu wenye hawakuoni kama binadamu hujui utaanza kuwaelezaje. Nilienda wakati mmoja nikapima maongezi yao nikaona hawanipendi na sijawahi rudi huko na pia watoto wangu huwa hawaendi. Naamini familia ya mume wangu hainipendi.

Jennifer aliongeza kuwa mwanawe ashawahi kabiliwa na shida fulani lakini scan hazikuwa zinaonesha chochote. Hapo wakampeleka kuombewa na mapepo yakaanza kujifichua.

Pepo ziliongea na mtu aliyetuma zikamtaja majina yake yote na walitaja ndugu ya mume wangu lakini wa baba tofauti.

Jennifer alisema kuwa ndugu aliyetajwa alikuwa tayari ameaga dunia.

Juhudi zetu za kumfikia bwana Aggrey hazikufua dafu na ilimbidi amtumie ujumbe.

Ningemwambia bado nampenda kama baba wa watoto wangu. Kama alitutenga basi asisahau watoto wake.