Pastor

NA NAOM MAINYE

Mhubiri mmoja kutoka Pokot Magharibi alikamatwa katika eneo la Ywateleke kwa kuwalazimisha watoto kuacha shule na kujiunga na kanisa Lake ambapo wanaabudu wakiwa uchi wa mnyama.

Samuel Kalwari kwa jina la majazi Eliya alisema kuwa alielekezwa na Mungu kuacha kazi yake ya uuguzi na kumtumikia Mungu. Hata licha ya kuwa muuguzi hakuwahusu wafuasi wake kutafuta matibabu hospitalini.

Mkewe Penina Lomatum alisema kwamba bwanake alitoka nyumbani Januari 2017 kwenda kazini. Alikuwa akirejea nyumbani kila wikendi kuona familia yake. "Nilipo oana, nilimwambia sitoshiriki kanisa lake na alinikubalia kushiriki katika kanisa langu. Nimegundua sasa kuwa ana jina jipya Eliya. Sikuwa na ufahamunalo." Alisema Lomatum.

"Nilisikia kwamba hatumii chumvi wala sukari na hatotumia noti mpya. Nilisikia kuwa alikamatwa na nikaamua kuja kumuona leo." Alisema.

Penina aliiomba serikali kulichunguza kanisa hilo kuhakikisha kwamba limesajiliwa na vile vile kuharakisha kufanya uchunguzi huo ili Kalwari arejelee kazi yake kulea wanawe.

"Sina kazi na nilikuwa ninamtegemea kuikimu familia yetu." Alisema mkewe. Kamanda wa polisi eneo la Kipkomo Mohamed Kofa alisema kuwa Kalwari alishikwa pamoja na wazazi wa watoto walioathirika.

"Tumemshika Samuel pamoja na wazazi wa watoto walioathirika na tunafanya uchunguzi kupata habari kuhusiana na kanisa hilo. Tunataka kujua wanachofanya wakiabudu uchi milimani." Alisema Kofa.

Mohamed aliwaagiza machifu kuhakikisha kwamba watoto wote wanaoenda shuleni wapo shuleni na wazazi wanaofeli kuhakikisha kwambo watoto wao wapo shuleni kushikwa.

"Wazazi wanaofeli kuwapeleka watoto wao shuleni wanafaa kushikwa na kushtakiwa kwa kuwa ni kinyume na sherai kutopeleka mtoto shuleni." Alisema Mohamed.

View Comments