Abiy Ahmed

Waziri mkuu wa Ethiopia  Abiy Ahmed  ameshinda tuzo ya mwaka huu ya amani ya Nobel . kamati  ya tuzo hiyo kutoka Norway imetoa tangazo hilo la kumpa Abiy  taadhima hiyo kwa ajili ya juhudi zake za kuleta amani kati ya Ethiopia na taifa jirani la Eritrea  kwa ajili ya mzozo wa muda mrefu wa mpakani . Ahmed alitajwa kuwa mshindi wa 100 wa Nobel Peace Prize huko Oslo.

Jumla ya washiriki 301 waliochaguliwa katika tuzo hizo zenye hadhi kubwa, washiriki 223 ni watu binafsi na kampuni 78 .Tayari watu walikuwa wamekisia nani angeshinda tuzo . Chini ya kanuni za asasi ya Nobel , washiriki waliotajwa majina yao hayaruhusiwi kuchapishwa kwa miaka 50.

View Comments