mbwana samatta

Ni likizo ya kimataifa na wachezaji wenzake wengi wapo katika zamu ya kimataifa lakini nahodha wa timu ya Taifa Stars na KRK Genk Mbwana Samatta alikuwa na mipango mingine kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania.

Mshambuliaji huyo matata alitumia wakati wake mzuri wa likizo hiyo siku ya Alhamisi kufunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi Neima Mgange.

Sherehe ya harusi yake iliofanyika katika kijiji cha kijichi mjini Dar es Salaam ilihudhuriwa na wachezaji wenzake wa Taifa Stars akiwemo Himid Mao na Thomas Ulimwengu kulingaa na gazeti hilo.

Ilikuwa sherehe ya kufana miongoni mwa watu wa familia ya Mgange walipokutana na mshambuliaji huyo ambaye ndiye mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kushiriki katika ligi ya mabingwa Ulaya.