- alyxok4qpejozo85ng5d9a2d6a5e594
- download

Baada ya jitihada za kuitoa gari na miili ya Mariam na mtoto wake kufaulu, sasa ni jukumu la asasi za usalama kuchunguza kisa hicho.

Katika mahojiano na kituo cha runinga cha NTV, mmewe Mariam John Wambua alitetea mkewe kuwa hakuna uwezekano wowote wa kurudisha gari nyuma na kutumbukia baharini.

Wambua alikuwa akikana taarifa kuwa huenda mkewe alikuwa na njama ya kujiua pamoja na mtoto wake.

Bwanake alisema kuwa gari la mkewe lilikuwa katika hali ya kuegeshwa huku akiwasihi wanapolisi kuharakisha zoezi la uchunguzi.

Haya yanajiri huku feri zilizopo katika kivukio hicho zikidaiwa kuwa mzee zaidi na zina zaidi ya miaka 30.

Kwa umbali, mabati ya feri hizo yana kutu kuashiria uzee.

Milango ya feri hizo na sehemu za kukanyagia unapoingia zimezeeka zaidi.

Wengi wanahoji kuwa hali mbovu ya feri pamoja na utepetevu kazini zilichangia pakubwa na kuwa ajali hii ingeepukika.

Aidha, nyufa za mamlaka ya feri nchini kukosa kuajiri wapiga mbizi ili waweze kusaidia kunapotokea ajali zimeonekana wazi.

Miili ya Mariam Kigenda na mwanawe wa miaka minne Amanda ilipatikana ikiwa imekumbatiana katika kiti cha nyuma ndani mwa gari lao.