RADIO JAMBO MIC

Familia za wakenya waliofariki katika ajali ya ndege ya  Ethiopia hatimaye zimekubaliwa kuichukua miili ya wapendwa wao . waziri wa mashauri ya  kigeni Monica Juma amesema miili yote  imetambuliwa huku 28 ikiwasili  nchini kwa maazishi ilhali iliosalia itachomwa.miili mingine ya waliokuwa na uraia wa zaidi ya nchi moja  itazikwa kwa mujibu wa matakwa ya familia .

Wazazi wameshauriwa kukoma kuwapa shinikizo wanafunzi kufanya vyema katika mitihani ya kitaifa .waziri wa elimu George Magoha  pia amewataka watahiniwa wa mwaka huu kutoitikia kuwekwa chini ya shinikizo kwani kila mmoja atasonga katika hatua ifuatayo ya elimu bila kujali matokeo yake .

TSC imewapiga marufukua walimu waliohusika na visa vya udanganyifu  katika mitihani ya hapo awali dhidi ya kusimamia mitihani ijayo ya KCPE na  KCSE . Afisa mkuu wa  tume hiyo  Nancy Macharia  amesema katika miaka mitatu iliyopita ,wamewachukulia hatua walimu 144 waliohusika na udanganyifu katika mitihani ya kitaifa .

Kiongozi wa walio wengi katika bunge  la kaunti ya  Nairobi Abdi Guyo  ameandikisha taarifa na DCI akidai kamba maisha yake yamo hatarini . Amesema kizazaa kilichotokea city hall wiki jana kilipangwa na magenge yalitumwa katika bunge la kaunti kusambaratisha shughuli .

Mshikilizi wa rekodi ya dunia katika mbio za marathon Eliud Kipchoge  ametaka kukutana na rais wa zamani wa marekani Barrack Obama .hii ni baada ya Obama kumtumia ujumbe wa kumhongera katika twitter  kwa kumudu kumaliza mbio za marathon chini ya saa mbili .Obama pia alimtambua  Brigid Kosgei kwa kuvunja rekodi ya akina dada katika mbio za marathon..Kipchoge anataka kukutana na Obama ili kujadili jinsi ya kuufanya ulimwengu kuwa bora zaidi .

Wakaazi wa Mombasa wanaitaka serikali kuboresha usalama katika feri  ili kuzuia maafa siku za usoni . wamesema baadhi ya  sehemu za feri zinafaa kuboreshwa na pia kuweka vifaa vya kuwawezesha watu kujiokoa wakati panapotokea  dharura .

View Comments