Angela

Katika kitengo chetu cha Ilikuaje na Bi Massawe Japanni, mhubiri mmoja ambaye alikuwa dansa alifunguka wazi kuhusu yaliyotendeka haswa siku ya kufa kwake marehemu Angela Chibalonza.

Jamaa huyu, jina lake John Isaji alisema kuwa, siku hiyo ilikuwa ni siku ya kawaida tu, siku iliyoanza kama kawaida na mipango yakiwa kama kawaida.

Kama ilivyokuwa desturi yake Angela Chibalonza kuwa na kesha mbalimbali za kuimba nyimbo zake za injili na kuhubiri, sikuĀ  ya kifo chake, mwanamziki huyu alikuwa amefunga safari kuenda Egerton University kuendeleza kazi ya Mungu.

Vilevile, John alizidi kusema kuwa, safari hiyo ya kuenda Egerton ilikuwa na mikosi chungu nzima na hata wakati wa kuenda hawakuwa na gari la kuwasafirisha mpaka kwenye chuo kikuu cha Egerton.

''Safari hii ilikuwa na changamoto sana kutoka asubuhi juu ilinibidi nitoke Egerton kitu 5 jioni niende mpaka Nairobi kutoka Nakuru ndiposa tusafiri mpaka Egerton.''John alisema.

Zaidi ya hayo, marehemu Angela Chibalonza pamoja na kikosi chake walikata shauri kutoenda kwenye kesha ile kwa sababu ilikuwa imefika usiku sana na hawakutaka kusafiri usiku.

Hata hivyo, wanafunzi wa chuo kikuu cha Egerton ambao walikuwa wanamsubiri Angela Chibalonza walizua vurugu na vurumai baada ya kuambiwa kuwa Angela ameahirisha safari yake.

John alisema kuwa, wanafunzi hawa walikasirika sana na kudai eti walikuwa wamechezewa shere na hapo ndipo Angela akaamua atasafiri vivyo hivyo mpaka Nakuru ili kuokolea maisha ya wengi waliokasirika.

''Wanafunzi wa Egerton waligoma na kukasirika sana baada ya Angela kusema kuwa ameahirisha safari yake.''

Angela walipofika Egerton, alimaliza kilichompeleka pale na wakti wa kurudi, akamwambia John abadilishe Dereva kwani anaona ni kama John amechoka.

''Angela aliniambia nibadilishe dereva kwa sababu nilikuwa nimechoka na kusema nikitaka alale nipeane gari.''

Hata hivyo, sikuwa namuamini dereva yeyote kwani ata kama nilikuwa nimechoka, sikutaka kubadilisha dereva.

''Kufika Nakuru, Angela aliniambia tena nisijaribu kuendesha gari lile tena kwani nilikuwa nimechoka na kuzidi kuwa she is not comfortable nikiendesha gari kama nimechoka.''John alisema.

Basi dereva mwingine alishika doria na kuanza safari na kwa vile John hakuwa amemzoea dereva yule alifunga mshipi wake lakini Angela hakuwa amefunga mshipi.
Basi amini usiamini, dereva yule alikuwa akipeleka gari lileĀ  kwa kasi sana na ghafla bin vuu gari hili likagonga lorry kubwa sana kutoka nyuma na mwanamziki Angela, dereva, na mwanahabari mmoja wakafariki.
John tu ndiye aliyenusurika.
Ama kwa hakika,ya mungu ni mengi.
Mungu ailaze mioyo ya marehemu Angela na wenzake mahali pema peponi.