IZKk9kpTURBXy81M2M1YWEyOTMyZDBjZDc5MjRjNzA5NGU2ZTkyNGE2MC5qcGeSlQLNAxQAwsOVAgDNAvjCw4GhMAE

Staa wa kike na mjasiriamali Akothee amefunguka mwanzo mwisho kuhusu hela anayotumia kwa mabinti wake.

Akothee ametangaza haya alipokuwa katika mahojiano na kituo kimoja nchini.

Kulingana na mwanamuziki huyu, mabinti wake hutumia kiwango cha laki mbili kwa mwezi.

Hii amesema huwazuia watoto wake kunaswa na wanaume wenye hela.

Ametangaza kuwa wasichana wake hawataweza kushirika katika ngono ili kuingiza pato.

https://www.instagram.com/p/B3qv3ylnN_1/

" Mimi huwapatia KSh 20,000 kila mmoja, sitaki wapitie maisha niliyoyapitia mimi, pia singependa wadanganywe na wanaume tajiri watakaotaka washiriki ngono nao...' Akothee.

Sio mara ya kwanza mama huyu wa watoto watano kujinadi na hela aliyonayo.

Aliwahi kudokeza kuwa yeye hutumia Kshs 2 Milioni ili kurembesha majumba yake ya kifahari.

Katika mahojiano, staa huyu alisema kuwa bidii na kujituma sana ni asili ya utajiri alionao.

’ Yanavutia (Majumba) maana kuna mtu ambaye anakosa usingizi akifikiria jinsi ya kuyarembesha. Natumia zaidi ya KSh 2 milioni kila mwezi kuhakikisha kuwa kila kitu ki shwari katika boma hizo.’’ Akothee.

View Comments