Katika kitengo cha Patanisho na Gidi na Ghost, jamaa mmoja bwana Morris alifunguka mwanzo mwisho na kusema kuwa walikosana na mke wake kwa sababu alimpata akizungumza na mpenzi mwingine.

Amini usiamini binti huyu alikuwa anatuma ujumbe wa kimapenzi kwa mpenzi mwingine huku akiwa na mumewe kitandani.

Morris alipomnyang'anya simu ile na kuona ujumbe anaotuma kwa wapenzi wengine, Morris aliamua kumzaba kofi na binti huyo akakata kauli kufunga virago vyake na kuenda kwao.

Mke wake Morris, Bi Pauline alipigiwa simu na Gidi na Ghost na alipoulizwa kama anamjua mume wake, alisema kuwa hamtambui na kukata simu.

Hivyo basi, bwana Morris na mke wake hawakupatanishwa.

Morris alipewa wosia na kuambiwa asife moyo kumpigia mke wake na kujaribu kurekebisha ndoa yake.

View Comments