RADIO JAMBO MIC

 Mbunge wa malindi Aisha Jumwa na mlinzi wake  wameagizwa  kufika mbele ya DCI  jumanne wiki ijayo  ili kuwasaidia  katika uchunguzi  kuhusiana  na rabsha zilizotokea katika wadi ya ganda na kupelekeea kuuawa kwa mtu mmoja . wameachiliwa kwa dhamana  kwa ajili ya ukosefu wa ushahidi .

Baadhi ya barabara  mjini Mombasa hazipitiki kwa ajili ya mvua kubwa  inayoshuhudiwa katika eneo hilo .idara ya utabiri wa hali ya anga  imesema kiasi cha mvua  kitazidi  huko pwani  hadi jumapili .

Wanafunzi  wawili waliopotea  kutoka shule ya  wavulana ya utumishi  huko gilgil  wamepatikana  wakiishi hapa Nairobi  na binamu zao  baada ya kutafutwa kwa wiki mbili . wawili hao ambao ni watahiniwa KCSE walitoweka kutoka shuleni humo katika hali ya kutatanisha .

Mswada wa punguza mizigo  umefeli na  sasa  wakenya wanafaa kuangazia jitihada za jopo la BBI . baadhi ya viongozi wanaounga mkono BBI wamesema   jitihada hiyo ndio njia bora  kwa taifa  kwani maoni ya wakenya wote katika kaunti 47 yalichukuliwa .

  Mbunge wa malindi aisha jumwa  Aisha jumw ana mlinzi wake  wameachiliwa huru kwa dhamana ya shilingi laki tano pesa taslimu au bondi ya shilingi milioni moja kila mmoja .mahakama  imekataa kuwazuilia kwa siku 21 kama  ulivyotaka upande wa mashtajka  kwa ajili ya kukosekana kwa ushahidi kuhusu mashtaka ya kuchochea ghasia .

Waziri wa afya Sicily kariuki  amefika mbele ya kamati ya bunge kuhusu afya ili kutoa maelezo kuhusu  ununuzi wa vifaa vya matibabu  uliosababisha kupotea kwa mabilioni ya pesa za umma . kariuki amewaeleza wabunge hatua kwa hatua kuhusu utaratibu uliofutwa katika ununuzi huo kuanzia mwaka wa 2015 .

Seneta wa Nairobi Johnson Sakaja  amewasilisha kesi  kuzuia kuteuliwa  kwa mary wambui kama mwenyekiti wa maamlaka ya ajira .amesema  wambui hana tajriba ya a angalau miaka saba katika uajiri  na usimamizi wa wafanyikazi ili kushikilia wadhfa kama huo kama inavyohitajika  sheria .

View Comments