kdf

Serikali siku ya Alhamisi ilitangaza kufutilia mbali usajili wa makurutu wa kujiunga na kikosi cha KDF baada ya wabunge kulalamikia zoezi kwamba linafaa kufanyika katika makao makuu ya kaunti ndogo sio tu katika makao makuu ya kaunti kama ilivyokuwa imeratibiwa.

Usajili huo ulikuwa umeratibiwa kuanza Octoba 7 hadi Novemba 7.

Wabunge walimuagiza waziri wa Ulinzi Raychelle Omamo kuhojiwa na kamati ya uhusiano mwema na Ulinzi ili kueleza sababu za kubadilisha mfumo na vituo vya usajili.

Wabunge wanasema kwamba mabadiliko katika taratibu za usajili yatatawafungia nje vijana wengi walio na ari ya kujiunga na kikosi cha jeshi kwa kuwa wengi wao hawana uwezo wa kufika katika makao makuu ya kaunti zao.

View Comments