Hivi leo katika kitengo chetu cha Patanisho na Gidi na Ghost,jamaa mmoja jina lake Titus alijitokeza na kusema kuwa amekosana na baba mkwe wake.

Akisimulia kisa chake na kilichomfanya akosane na baba mkwe ni kuwa,alikutana na binti ya baba mkwe huyu na kumpenda ata kabla amalize kidato cha nne akiwa na maazimio ya kufunga pingu za maisha naye baada ya kumaliza skuli.

Hata hivyo,siku moja alikuwa amemsindikiza binti huyu nyumbani usiku wakitumia pikipiki kisha familia yake msichana ikawaona na papo hapo wakazua vurugu na vurumai.

Mbona mtoto wao anaongea na jamaa usiku?

Zaidi ya hayo,jamaa mmoja aliyekuwa amewabeba na pikipiki alitaka kutoroka na pikipiki ile na hapo ndipo Titus aliamua kufanya vurugu akijaribu kuokoa pikipiki ile issibiwe na katika harakati zile, akamshtua nyanyake binti na tangu hiyo siku,baba mkwe akamkasirikia sana.

Amini usiamini,kwa sasa wapenzi hawa wana mtoto lakini bado baba mkwe hataki kuzungumza naye na akasema kuwa hatawahi msamehea Titus kwa sababu ya kujaribu kumuua nyanya.

Cha kusikitisha ni kuwa,baba mkwe alipopigiwa simu hakushika simu ya patanisho na kwa hivyo,Titus hakuweza kupatanishwa na baba mkwe.

View Comments