- lori.1.jfif
- lori.2.jfif
- lori.3.jfif

NA SOLOMON MUINGI

Watu wawili walifariki mapema siku ya Jumatano baada ya lori kupoteza mwelekeo na kutumbukia kwenye mto eneo la Sisera kwenye barabara ya Voi kwenda Mwatate, kaunti ya Taita Taveta.

Kamanda wa polisi katika eneo la Mwatate Monicah Kimani alisema lori hilo lilipoteza mwelekeo katika daraja la Mtwamwagodi na kutumbukia mtoni.

Alisema dereva wa lorihilo na msaidizi wake waliaga dunia papo hapo. Ametoa wito kwa madereva kuwa wangalifu na kujiepusha na uendeshaji magari kwa kasi mno.

Kamanda huyo wa polisi alisema hakuna kitu kilikuwa mbele ya gari hilo na kuongeza kuwa dereva alishindwa tu kulidhibiti kwa sababu alikuwa kwa kasi ya juu. Kulingana na Kimani ni rahisi kulidhibiti gari likiwa katika kasi ya kadri.

“Kupoteza control na ni self involved hakuna kitu ambacho kilikuwa mbele yake, that must be over speeding”.

Alisema kwamba waliofariki na wa umri wa kati ya miaka 20 na 24.

View Comments