uhuru.birthday

Hii leo ikiwa maadhimisho ya miaka 58 tangia rais wa nne wa jamhuri ya Kenya, mheshimiwa Uhuru Kenyatta azaliwe, wakenya wengi wamechukua fursa hiyo kumtakia heri njema akiwemo naibu wake, William Ruto.

Ruto kupitia mtandao wa Twitter, alimtumia bosi wake ujumbe mfupi akimtakia baraka tele.

Hata hivyo, katika ujumbe wake, alimsifu Uhuru kwa kuwa mtu aliyempa yeye na mamilioni ya wakenya msukumo mkuu kwa kuwa rais mchanga zaidi nchini.

Ujumbe huo haukuishia hapo kwani alimalizia kwa kumkumbusha mkuu wake kuwa anangoja siku watakapostaafu ili wawili hao wafanye walichokubaliana.

Ruto aliandika,

Happy birthday to my friend & Boss H.E. Uhuru Kenyatta. You are a great inspiration to me, Jubilee leadership and millions of Kenyans as the youngest President we've ever had. As we age, I look forward to what we agreed on to do when we retire. Remember? Ubarikiwe mpaka Ushangae!