janet mbugua

Kama kuna mwanahabari ambaye tunaweza sema bila kusita kuwa amekuwa kielelezo chema kwa mamilioni ya watu humu nchini kwa ustadi na utendakazi wema, basi ni Janet Mbugua.

Kwa kazi nzuri na bidii yake, kwenye utangazaji na pia nje ya uanahabari, hamna asiyelijua jina lake kufikia sasa.

Alipojiunga na runinga ya Citizen mnamo mwaka wa 2011, yeye na mtangazaji mwenza, Hussein Mohammed waliunda majina yao na uhusiano wao hewani uliwavutia watazamaji wengi.

Hata hivyo, baada ya miaka mingi akifanya kazi Citizen, aliwashtua wengi alipotangaza kuwa atawachana na kazi ya kusoma habari, kwani tayari alikuwa ameguza maisha ya wengi, kutoka watoto hadi wazee.

Lakini swali ni je, mbona akaamua kuwacha uanahabari wakti ambao meli yake ilikuwa tayari imeng'oa nanga?

“Nilikuwa napitia uchovu mwingi kwa takriban miaka 10. Sikuwa na ule uhusiano wa karibu na mwanangu Huru. Nilikuwa nafanya kazi ya mzazi ya kawaida lakini msaidizi wangu nyumbani ndiye aliyefanya kazi kuu. Kuna wakati nilienda kumkumbatia mwanangu na akasongea mbali na hapo ndipo nikagundua kuwa mambo sio mazuri.

Hapo nikapanga mapato yangu kwa kipindi cha miezi sita kuhakikisha yako sawa na nikapanga na nikapanga miradi ambayo yangenitosheleza kwa angalau miaka miwili." Janet alisema katika mahojiano na Betty Kyallo.

Sasa hivi amesema anazingatia imani, familia yake na kuwa mkamilifu.

View Comments