hamronizze_420x315__1572252837_55071

Kikundi cha wanahabari nchini kimeachwa na mshangao mkubwa na kudai kuwa Harmonize alionyesha dharau kubwa kwao.

Staa huyu alitalii nchini katika mchakato wa kupigia debe nyimbo yake mpya ya Uno.\

Harmonize ambaye amepanga msururu wa safari katika nchi mbalimbali kuipa nguvu ngoma hii alisubiriwa na wanahabari hao kwa masaa mengi.

Konde alizungumza kwa dakika 3 na kuondoka na kuwaacha wanahabari.

Jeshi alitakiwa kuhutubia kikao hiki cha wanahabari kabla kuendelea na safari yake.

Katika ziara hii, Harmonize C.E.O wa Konde Gang anapania kuipeleka nyimbo ya Uno hadi iwafikie watu wa tabaka mbalimbali.

Ngoma ya Uno inafanya vizuri katika mtandao wa YouTube muda mchache tu baada ya kutoka.

Harmonize alianza safari hii na gang yake nchini Tanzania.

https://www.instagram.com/p/B4FatHDnLvb/

Alionekana kufunguka zaidi katika mahojiano na vituo vya utangazaji nchini humo tofauti na hapa Kenya.

Alimwaga mtama wote A-Z kuhusu lebo ya WCB na baadae akafanya party kubwa ya wanahabari huku akiperform Uno.

Kikao chake na wanahabari Kenya kilisubiriwa saa tano mchano na baadae akasukuma hadi saa tisa alasiri.

Kikao hicho baadae kilisongezwa hadi saa moja jioni. Hii ina maana kuwa wanahabari hao walimsubiri siku nzima.

Je, unadhani ni kitu gani kilimfanya Mmakonde huyu kuwazimia data wanahabari Kenya?

Kama desturi za vikao hivi, wanahabari walikuwa washatua eneo la Blue Door VIP lounge kumsubiri staa huyu.

Kwa tendo la kejeli zaidi, walinzi wa staa huyu walisukuma viti na kumpisha atoke kwenye kikao.

Mtangazaji wa runinga alikerwa na kiburi hiki na kusema,

“Huyu jamaa ako na madharau sana, hutawahi niona kwa event ama press conference yake tena”

Mwingine aliongeza,

"Hivi sivyo mtu anavyopaswa kuishi na watu, hususan vyombo vya habari. Atajua hajui. Kiburi chake hakiwezi kumpeleka mbali. Hakuna siku moja hivi nitafika kuangazia chochote kinachomhusu..."