unnamed__3___1572347718_38555

Rabsha zimezuka katika bunge la kaunti ya Nairobi kwa mara nyingine.

Vurugu hizi zimetokea baada ya wawakilishi wodi kukosa kupatana kuhusu mswada wa kumfurusha afisini spika wa bunge Beatrice Elachi.

Kizaazaa kilianza wakati wawakilishi wodi wanaounga mkono Elachi waliwafumania wenzao wanaounga mkono kiongozi wa wengi Abdi Guyo.

Ngumi na teke zilitembea katika bunge hilo wengi wakionekana kutafuta pa kuhepea.

Hii sio mara ya kwanza vita kutokea katika ofisi za bunge la kaunti ya Nairobi.

Wawakilishi wanaomuunga mkono Guyo walikuwa wameita kikao na waandishi wa habari.

Kikao hiki kilikuwa na nia ya kuwajibu wenzao waliotishia kwa idadi kubwa ya watu bungeni.

Mawe, chupa za maji vilionekana kurushwa katika mtifuano huo.

Mwakilishio wodi Nairobi magharibi Maurice amesema kuwa wenzao wa ODM hawatahusika katika mswada wa kumfurusha Elachi.

“Kama chama tuna msimamo, kama wawakilishi wodi tunaunga mkono Elachi kama spika..." Maurice.

View Comments