massawe

Vita, vurugu, mateso na hata ubakaji ndani ya ndoa ni visa ambavyo vimeripotiwa sana ndani ya ndoa na kama chanzo kuu cha kuvunjika kwa ndoa na familia nyingi kote duniani.

Kwa hivyo ni jambo la kueleweka kila unaposkia kuwa wapenzi fulani walitengana kwa ajili ya mojawapo ya visa hivyo.

Hata hivyo, wanajambo waliwachwa na mshangao pindi mwanadada mmoja kwa jina Maureen, alipofichua kuwa vita ndani ya ndoa yake ni jambo linalo ashiria upendo na isitoshe ni jambo la kawaida.

Maureen na mumewe wa miaka mitano wamejaliwa mtoto wa miaka mitatu, lakini wao wamekuwa wakipigana kila wiki na wasipopigana yeye hujua kuwa mambo sio mazuri na huenda akawachwa.

Soma usimulizi wake bi Maureen,

Sasa mimi nina mwanaume tusipopigana najua kuna shida na sisi hupigana kwa mangumi na mdomo. Tusipopigana na akuje aketi hapo kama padri mimi hujua kuna tatizo, kama kuna mahali nimemkasirisha na anataka kuniacha.

Lakini tukipigana najua tuko sawa kwani kila wiki lazima tupigane, lakini sio kupigwa ila kupigana kwani mimi siwezi pigwa.

Na sisi hupigania kitu kidogo kwani tuseme ameingia kwa nyumba mbele yangu na nimpigie simu niskie amefika, mimi hujua tayari lazima tupigane.

Juu akishaniuliza nilikuwa wapi nikimuelezea ananizaba makofi nami naamka tunaanzana halafu baadaye tunaketi chini tunazungumza na hayo yanaisha, hata nimezoea.