- Milly-Chebby-tells-off-her-haters-600x600
- terence

Ubuyu wa Terrence Creative kuhusika katika tendo la ndoa na mpango wa kando wa miaka 19 ulisambaa katika mtandao kama moto jangwani.

Terrence Creative baadaye alikiri kuwa alimsaliti mkewe Milly Chebby na kuomba msamaha.

Wafuasi wa Terrence hawakupendezwa na msamaha alioutoa kwa mkewe.

Ubuyu huu pia ulionekana kumchonganisha na kumuweka kwenye kiti moto Anita Soina.

https://www.instagram.com/p/B4YAUp_hhRJ/

Inadaiwa kuwa Terrence alichepuka na Anita Soina kisa na ambacho hakikumfurahisha mkewe Milly Chebby.

Kumewaka moto pia katika DM ya Insta ya Milly Chebby baada ya kujulikana kuwa alitumia njama za kumtishia na kumtusi Anita Soina ili kuinusuru ndoa yake.

Chebby amefikia levo za kumtishia kuwa atatuma kundi haramu la Mungiki kumvamia.

Kwa kauli hiyo, wafuasi wake walizamia Insta yake na kuangusha cheche za matusi kwake.

Chebby ameonekana ku-mind sana wanachokisema na kuwajibu kwa Insta Story yake.

"Jumbe za kunitusi kwa sababu ya unene wangu sio tishio nipo sawa...."

"Nitafika Gym kwa wakati wangu..." Alifoka Chebby.

View Comments