mariga

Mgombea wa Jubilee, McDonald Mariga amewaahidi wananchi kuwa ataskuma mswada wa kuhalalisha bangi iwapo atachaguliwa kama mbunge wa Kibra.

Mariga alikuwa anazungumzia mkutano wa kisiasa katika uwanja wa Laini Saba, Kibra, jumapili kabla ya uchaguzi mdogo utakaofanyika siku ya alhamisi.

Kwa siku mbili zijazo, watu 118,658 waliojiandikisha kama wapiga kura wanatarajiwa kupigia kura mmoja kati ya wagombea 24 kuwa kama mbunge wa Kibra.

Uchaguzi huo mdogo utafanyika kufuatia kifo cha Ken Okoth, ambaye aliaga baada ya kuugua ugonjwa wa saratani.

“Mnataka tuongelee mambo ya shada. Tunajua shada inacure cancer. Hio lazima tuipush. Shada si ni medicine? Sasa mimi nataka muniingize bunge tuanze kutetea hiyo mambo ya shada." Alisema.

Okoth alikuwa amepanga kupeleka mswada wa bangi bungeni mwaka wa 2018 akitaka ukuzaji wa bangi uhalalishwe.

Katika pendekezo lake kwa spika wa bunge, Justin Muturi, Okoth alitakaa hatua za msamaha kuanzishwa ili kuondolewa kwa rekodi za uhalifu dhidi ya raia walio na hatia ya utumiaji wa bangi.

Mariga aliahidi kubadili maisha ya wakaazi wa Kibra kwa kuunda kazi zaidi.

"Wao (ODM) wametutusi lakini tutaendelea kurekebisha maisha. Tunataka kupunguza idadi ya vituo vya polisi huko Kibra kwa kuunda njia zaidi za kazi," alisema.
View Comments