- video_timmy_tdat_x_rosa_ree_vitamin_u__1573036216_13811
- video_timmy_tdat_x_rosa_ree_vitamin_u__1573036267_35154
Rapa wa kike Rosa Ree amefunguka kuhusu video chafu aliyoifanya na TimmyTdat.
Katika mahojiano na ripota wa Bongo 5 nchini Tanzania, rapa huyu ametoa radhi kwa mashabiki wake waliokwazika kwa kutazama filamu hiyo.

"Kwanza ningependa kuomba radhi kwa video ambayo imekuwa ikisambaa mtandaoni. Ninafurahi kwamba nimepita wito kutoka kwa bodi ya filamu Tanzania."

Aidha, kampuni ya YouTube iliitoa video hii katika akauti ya Timmy.

https://www.instagram.com/p/B4eiJbLnL7K/

Vitamin U ni ngoma ya Timmy T Dat aliyomshirikisha Rosa Ree na ilisheheni vipande vyao wakiwa uchi kwenye bomba la maji.

"Ningependa kuomba radhi kwa waliokwazwa na ile video iliyosambaa mtandaoni. Leo hii nimefurahi kukutana na Bodi ya Filamu Tanzania 🇹🇿  na wamenielimisha mengi kuhusiana na sanaa na kanuni zake. Tutaendelea kufanya kazi pamoja ili kuweza kuifikisha sanaa ya Tanzania mbali zaidi." Alichapisha Insta

Katika video hiyo dakika 3 na ushei, Timmy T Dat anaoenakana akishika sehemu za siri za mwanadada huyu.

Rosa Ree amesema kuwa alifahamu mengi kutokana tukio hilo,

"Na wameweza kunielimisha mambo mengi sikuwa nayafahamu kuhusiana na sanaa ya Tanzania pamoja na bodi yao pia."

"Nimefahamu kuwa natakiwa nipeleke script yangu ya video kabla sijaachilia."

"Pale nitaweza kupata kibali baada ya wao kukagua vizuri na kupitisha script.."

"Niseme pole kwa wale waliokwazwa na video iliyosambaa."