David Lang'ata

Mshukiwa moja anayetuhumiwa kuwahonga wapiga kura katika kituo cha Mashimoni amekamatwa na polisi katika uchaguzi mdogo wa Kibra unaoendelea.

Davidi Korir ambaye ni mfanyakazi katika afisi za CDF za Lang'ata alikamatwa na noti za shilingi 200.

Anadaiwa alikuwa akimpa kila mpiga kura noti hizo tano, idadi hiyo ikifika shilingi 1000.

Mpiga kura mmoja alionyesha ithibati kuwa alikuwa amepokea kitita hicho kutoka mshukiwa.

‘Pesa ndiyo nimeishika. Kama mnajua mko na kura mbona mnaleta hapa pesa zenu za njaa njaa!" mwanamke aliimbia kituo cha NTV.

Afisa mkuu wa polisi wa  kanda ya Nairobi Philip Ndolo amesema kwamba mshukiwa yupo kizuizini huku uchunguzi ukiendelea ili kubaini madai hayo.

"Mwanaume huyo amekamatwa na uchunguzi kubaini madai hayo ya kuhonga wapiga kura umeanzishwa," Ndolo alisema.

Kwingineko afisa wa IEBC ambaye alikuwa ameratibiwa kuhudumu katika kituo cha Woodley amekamatwa.

Mwanaume huyo anatuhumiwa kwa kupokea kitita cha maelfu ya pesa kupitia M-pesa.

"Mshukiwa yupo kizuizini na uchunguzi kubaini madai hayo umeanzishwa," Ndolo alisema.

Bernard Okoth wa ODM ambaye ni kakake marehemu Ken Okoth wanakabiliana na mgombeaji wa Jubilee McDonald Mariga ambaye alikuwa mchezaji soka.

Miongoni mwao ni Eliud Owalo wa ANC na wagombeaji wengine 24.

View Comments