EIniLgAXkAA-Ij3

Mgombezi wa ubunge MacDonald Mariga hatapata nafasi ya kujipigia kura uchaguzi wa leo Kibra.

Zoezi la upigaji kura ilianza mapema leo asubuhi katika vituo 5 vya eneo bunge hili.

Kwa mujibu wa rejista ya wapiga kura Kibra, mgombezi huyu sio mpiga kura.

Mariga aidha ametokeza katika kituo cha kupiga kura Lindi ila hajaweza kupiga kura.

Staa huyu wa soka ni mpiga kura eneo bunge la Starehe.

Kifungu cha sheria kipo kwamba ni lazima mtu apige kura katika kituo alichorejista.

Uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Kibra unawavutia jumla ya wagombeaji 24.

Zoezi hili linaendelea huku wakaazi katika eneo hilo wakiwa na azma ya kuchagua mbunge wao kati ya wagombea ishirini na wanne waliojitokeza katika kinyang’anyiro hicho.

Kiti cha ubunge katika Kibra kiliachwa wazi baada ya kifo cha aliyekuwa mbunge Ken Okoth.

Mgombea wa chama cha Jubilee McDonald Mariga , Eliud Owalo wa ANC na Benard Okoth wa ODM wamekuwa wakiangaziwa sana kutokana na umaarufu wa vyama vyao.

Je,unadhani ni nani ataibuka kuwa mshindi Kibra?

View Comments